Nimefanya mazungumzo na baadhi ya wakazi kutoka Wadi ya Sabaki, wanaolilia kupata haki ya kipande chao cha ardhi cha zaidi ya ekari 200 eneo la Sabaki- Bridge. Wamekuwa wakiishi katika kipande hicho kwa zaidi ya miaka 80 na sasa wanahangaishwa na baadhi ya watu wanaodai kuwa ni mali yao.
Naahidi kutatua tatizo lao kisheria, na tuko na kamati ya ardhi ya Kaunti iliyochaguliwa kupitia kwa wakili mkuu wa Kaunti. Tayari imeanza kutekeleza jukumu lake la kupitia shamba hadi shamba ili kunakili utata uliopo na kupata stakabadhi zote kuhusu shamba hilo ili tupate mwelekeo na hatimaye kutafuta suluhu la kudumu.
Nimetoa kauli mara si moja kuwaonya mabwenyenye wanaowahangaisha wakazi hapa Kilifi kwenye ardhi wanamoishi na narudia tena, sitakubali kwa njia yoyote ile kuangalia Wananchi wangu wakihangaishwa na endapo kutakuwa na thibitisho la dhulma zozote zile, basi ardhi hiyo itarudi mikono salama ya Wananchi wa Sabaki- Bridge.