Nimezipokea kwa mshtuko na maskitiko taarifa za kifo za aliyekuwa Chifu wa kata ndogo ya Dabaso, Maitha Baya wa Kachelele, kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika eneo la Msabaha mapema leo.
Kwa mara nyengine tena, jinamizi la ajali limetuachia pengo kubwa katika jamii yetu. Nawaomba madereva wote kuwa waangalifu zaidi wakati mnapoendesha magari, ili kupunguza idadi ya ajali za barabarani. Kama jamii tumepoteza Baba aliyekuwa mshauri, mpenda elimu na maendeleo, mwenye utu, bidii na zaidi muungwana.
Naiombea familia na jamii nzima ya Kilifi kwa jumla, faraja na subra katika kipindi hiki kigumu kwa kumpoteza kiongozi huyu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema penye wema