Nimetembelea na kutoa rambirambi zangu na za Gavana Gideon Maitha Mung’aro kwa familia ya mwendazake Risley Kavu (43) katika eneo la Ganga, Wadi ya Rabai Kisurutini kabla ya mazishi yaliyoratibiwa hapo kesho.
Maisha ya mwendazake yalikatizwa baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani huko Chakama, eneo bunge la Magirini alipokua akiishi na kuendeleza shughuli zake za kiuchumi.
Makiwa kwa familia na Mwenyezi Mungu awape nguvu katika wakati huu mgumu wa maombolezo na ailaze roho ya mwendazake mahali pema peponi.