Hii leo, maafisa wetu wa usalama wamefanikiwa kunasa na kuteketeza zaidi ya gunia 10 za muguka kufuatia msako mkali ulioendelezwa katika sehemu za Malindi, Adu, Mtwapa, Kilifi Kaskazini, Mariakani na Gongoni.
Shukran za dhati kwa wakazi wa Kilifi ambao wameendelea kushirikiana nasi kwa kutupa habari muhimu kuhusu wale ambao wanaendelea kukiuka agizo tulilotoa la kupiga marufuku utumizi na uingizaji wa bidhaa hiyo Kilifi. Naamini kwa pamoja, tutamaliza jinamizi hili na kuokoa vijana wetu.