Utamu wa Watamu unazidi kuwa tamu. Barabara ya Aquarius ikielekea ufuoni, Twaha road, Timbo Taka, Chini ya Mti, Bwana Kheri na M’mbuyu road tumezimaliza kuweka cabro na tayari tumeanza barabara ya kutoka shule ya msingi ya Jimba kuelekea zahanati ya Jimba.
Bado kuna barabara kama vile ya Baraccuda ambayo tumeiweka kwenye mpango na nyengine nyingi ndani ya mji huu wa kitalii. Naamini kwa kufanya hivyo, tutaimarisha sekta ya Utalii ambayo ndio uti wa mgongo katika eneo hili. Watamu ikiwa tamu, sisi tunakoleza utamu, utamu wa Mung’aro wa Kilifi!