Wakazi wa Ganze, tumesikiliza kwa makini mawazo yenu na tunasema ahsante. Tunafahamu changamoto za Ganze ni nyingi kama mlivyotueleza, ila kupitia uongozi wangu, naamini tutatoa suluhu kwa baadhi ya yale yanayowakumba ikiwemo swala la maji, miundomsingi ya shule za chekechea na barabara.
Tayari nimeamuru wauzaji wote wa maji ya vioski ambao walikatiwa mita, watembelee afisi za maji Kilifi ili waandikishane mkataba wa kulipa madeni yao polepole na warudishiwe mita zao za maji ili waendelee na biashara zao kama kawaida.
Hoja nyengine za uboreshaji na ujenzi wa masoko, huduma bora za matibabu, elimu na mengineyo, tutashughulikia kama tulivyoahidi. Shukran za dhati kwa Mbunge wa Ganze, Mheshimiwa Keneth Kazungu Tungule na mwenzako wa Magarini, Mheshimiwa Harry Garama Kombe, kwa kuungana na sisi kwenye mdahalo huu na wakazi wa Ganze.
Muhaswe zhomu anatsi aa Ganze!