Kwenye awamu yetu ya pili ya mradi wa KEMFSED, leo hii tumepeana maboti 31 ya kisasa yenye thamani ya zaidi ya shillingi millioni 84 kwa vikundi mbali mbali vya wavuvi mjini Malindi.
Hii ni katika juhudi zetu za kuendelea kuboresha sekta ya uvuvi kaunti ya Kilifi, ambapo mpaka sasa kwa jumla, tumefikia vikundi 135 kupitia KEMFSED, ikijumuisha vikundi vya ukulima, ufugaji, mazingira, ununuzi wa majokofu ya kuhifadhia samaki pamoja na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi kwa gharama ya shillingi millioni 380.
Inanipa furaha kwamba, vikundi tulivyovikabili vifaa kama hivi katika awamu ya kwanza, tayari vimeandikisha faida ya zaidi ya shillingi millioni tatu kutokana na mauzo ya samaki, na naamini kupitia kwa ufadhili huu, mapato ya wavuvi wetu yataendelea kuongezeka na kuimarisha uchumi wetu.