Haijalishi mti una urefu au upana kiasi gani, kwa mti wowote ule kunawiri, kuna mtu lazima alichukua muda wake mwingi kuutunza kwa kuupa mazingira bora katika kipindi cha ukuaji wake.
Wakati tunapoadhimisha siku ya upanzi wa miti hii leo, ningeomba tusipande miti tu bila kujali ukuaji wake, tuwe katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tunatunza miti yetu maana ndio uhai wetu.