Safari hii, lazima sauti ya mkazi wa Kilifi isikike kutoka kule mashinani na sitachoka kuwashirikisha Wananchi kwenye midahalo ya kuzungumzia kuhusu swala la utoaji wa huduma na miradi yote ya serikali ya kaunti.
Ahsanteni sana Magarini kwa kutenga muda na sisi na kujadiliana maswala muhimu, nawaahidi kwamba tutatekeleza hoja zenu muhimu ikiwemo swala la maji, afya na kilimo ili tuzidi kuboresha Kilifi yetu. Kilifi kung’ara yahitaji nikuskie wewe, na sauti yako itatusaidia kuijenga zaidi kaunti yetu.