Nimepata fursa ya kufanya vikao na baadhi ya wakazi wa Shakahola huko Adu Magarini, wakinielezea baadhi ya changamoto wanazopitia kama jamii.
Katika mazungumzo hayo yaliyoongozwa na Shadrack Baya na Joshua Mutinda, wamenieleza kuhusu miundombinu duni ya chuo cha kiufundi cha Shakahola na nimeagiza kuanza kwa ukarabati wa chuo hicho mara moja kuanzia Jumatatu juma lijalo, baada ya paa lake kung’olewa na upepo mkali na kusitisha shughuli za masomo kwa zaidi ya wanafunzi 200.
Aidha, baadhi ya barabara ambazo zimekuwa katika hali mbaya eneo hilo, zitaanza kukarabatiwa na pia juma lijalo, nitatuma maafisa wangu kutathmini sehemu bora tutakayojenga vyoo vya umma eneo hilo.