Kupitia mradi wa KEMFSED, nimefungua rasmi shule ya chekechea ya Habura eneo la Bombi, Adu Magarini, ikijumuisha jumla ya madarasa matatu, vyoo vinne pamoja na madawati.
Kukamilika kwa madarasa hayo kutawapa afueni takriban wanafunzi 100 ambao kwa muda mrefu, wamekuwa na miundombinu duni ya shule hiyo huku tayari nikiagiza wizara ya elimu kuajiri walimu wote ambao wamekuwa wakifunza na kulipwa na wazazi katika shule hiyo, sasa wataanza kulipwa na serikali ya kaunti.
Hii ni katika juhudi zetu za kuhakikisha kuna usawa katika jamii kupitia elimu na mradi sawia na huu, kwa sasa unaendelea katika shule ya msingi ya Ngoloko, Wadi ya Mtepeni, Kilifi Kusini.