Nimezindua rasmi mpango wa usambazaji wa mbegu ya mahindi tani 66 na mbolea bila malipo, zikiwalenga wakulima zaidi ya 11,000 kaunti hii. Pembejeo zitasambazwa katika Wadi zote 35 na zimegharimu serikali ya kaunti kima cha shilingi milioni 100, lengo ni kusaidia wakulima wetu kuzalisha chakula cha kutosha.
Tuko na changamoto ya tingatinga, mengi yamekuwa katika hali duni na hayawezi kuwafikia wakulima wote, lakini nimeweka mpango wa kununua tingatinga mpya na kukarabati baadhi ili ziweze kutoa huduma bora na kwa wakati unaofaa. Kwa wakulima nawahimiza kuwa na desturi ya kuandaa mashamba yenu mapema ili msimu wa mvua ukianza, mashamba yawe tayari kwa upanzi.