Kwa sasa ujenzi wa daraja la Kamkomani huko Mariakani eneo bunge la Kaloleni umefika asilimia 95. Mara tu utakapokamilika, wakazi wa Tonolo na Muungano watakuwa na urahisi wa kufika katika zahanati ya Kamkomani na maeneo mengine.
Awali, akina mama wajawazito pamoja na wagonjwa wa maeneo haya wangelazimika kusafiri mwendo mrefu zaidi kufika katika zahanati ya Kamkomani, lakini ujenzi wa daraja hili lililokuwa likisombwa na maji mara kwa mara,utawapa afueni, wakitumia wastani wa dakika 15 tu.