Nimejadiliana kwa kina na Wazee wa Muungano wa Mijikenda Elders Association, wakiongozwa na mshirikishi mkuu eneo la Pwani Tsuma Nzai Kombe, kuhusu sherehe za mwaka huu za ‘Chenda Chenda’ zitakazofanyika katika eneo bunge la Kaloleni, Kilifi.
Kama kaunti,tumejipanga kikamilifu kuleta pamoja jamii zote za Mijikenda eneo la Pwani, Kenya na Ulimwenguni kote katika sherehe hizi. Hii huwa ni fursa ya kuonyesha na kuendelea kukuza utamaduni wetu. Na matumaini makubwa yakutangamana na jamii yote ya Mijikenda, tujadiliane na tuweke mustakabali kuhusu maswala yanayotuhusu.