Nimeweka sahihi sheria ya uidhinishaji wa matumizi ya Kaunti ya Kilifi ya mwaka wa 2024 (Kilifi County Appropriation Act, 2024)
Kupitia sheria hii, shughuli za serikali ya Kaunti ya Kilifi sasa zinatarajiwa kuendeshwa kikamilifu na kutekelezwa kwa makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha 2024/2025.
Sheria ya matumizi ya fedha inatoa nafasi kwa bajeti iliyoidhinishwa, kuipa mamlaka husika jukumu la kufanya matumizi na kukusanya mapato kwa idara za serikali ya Kaunti.