Malindi imesikika, jinsi mlivyopaza sauti zenu imenidhirihishia wazi kwamba bado tunahitaji kunyorosha baadhi ya idara zetu ili huduma ziwafikie ipasavyo na nawahakikishia kwamba, si Malindi tu, Kilifi hii itanyoroka hasa katika swala la kumhudumia mkazi wa Kilifi.
Mwananchi wa kaunti hii hafai kuhangaika kutafuta huduma yoyote ile ya serikali, ni haki yake kikatiba na midahalo hii inazidi kunipa taswira ya zile idara ambazo zinafaa kuwajibika zaidi. Usafi wa mji wa Malindi unafaa kuwa wa masaa 24 kwa utalii wetu, swala la ardhi tunaendelea kulitatua, miundombinu bora ya barabara, afya na kilimo ni baadhi ya sekta muhimu katika mji wa Malindi ambazo kama serikali ya kaunti, tutazidi kuziboresha.
Nikifika kwako usinyamaze, maana Kilifi hii lazima tuing’arishe sote. Ahsanteni sana Malindi