Magarini, Malindi, Kaloleni, Kilifi Kusini, Kilifi Kaskazini, Ganze na sasa leo Rabai, tumeskia sauti zenu, na pia nashkuru jinsi mlivyoelezea kufaidika na miradi na huduma zetu ambazo tumetoa kwa muda wa miaka miwili sasa.
Pale mumetushauri tukaze kamba, nawaahidi, kwa ushirikiano na baraza langu la mawaziri, maafisa wakuu na wajumbe wetu wa bunge la kaunti, sitawaangusha. Nikirudi tena mashinani kwa awamu nyengine, na uhakika, asilimia tisini ya yale mliyotuagiza tufanye, tutakuwa tumekamilisha.
Tumecheza pamoja, tumecheka pamoja, tumekula pamoja tukafurahi pamoja. Tumezungumza na nyinyi kuhusu mafanikio na changamoto zetu zinazotukumba, na sitachoka, baada ya kutekeleza yale mliyotutuma sasa, nitarudi tena na safari hii nitaenda Wadi baada ya Wadi mpaka tumalize zote 35, tupige gumzo pale chini mashinani ya jinsi tutakavyoendelea kuing’arisha Kilifi yetu.