Vikosi vyetu vya ulinzi vina jukumu muhimu katika kutulinda. Nilikutana na wanachama wa Chama cha Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi (DEFOCA) wakiongozwa na Brigedi. J. N. Mwamburi, Mkurugenzi Mkuu wa DEFOCA, kujadili jinsi tunavyoweza kushirikiana kwenye miradi endelevu inayoweza kuwapiga jeki.
Kikosi hicho kina mipango yakuanzisha kantini na ujenzi wa jumba la mikutano, pamoja na miradi mengine ili kuwanufaisha wanachama pamoja na hata jamii.
Utawala wangu umejitolea kuunga mkono juhudi hizi, na kwa sasa tunatafuta ardhi ili kuwasaidia waweze kuwekeza miradi yao.