Tunaleta sura mpya ndani ya Hospitali ya Manispaa ya Muyeye mjini Malindi. Ujenzi wa vyumba 20 vya kujifungua kwa akina mama wajawazito umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95. Aidha, ndani ya Hospitali hii, tumejenga vyumba viwili vya upasuaji vya kisasa.
Hospitali hii sasa itapunguza msongamano wa akina mama wetu wanaotafuta huduma za kujifungua katika Hospitali kuu ya Malindi. Lengo langu ni kuhakikisha tunaboresha huduma zetu za afya. Kamwe sitachoka kuwahudumia wakazi wa Kilifi, hapa ni kazi kwenda mbele!