Nimewatembelea baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya mjini Kilifi, ambapo kambi ya siku mbili ya utoaji huduma za bure kwa wagonjwa imekamilika leo.
Kwenye kambi hii, tuliwaleta pamoja wataalamu wenye ujuzi katika upasuaji ambapo kesi za upasuaji zilizokosa kushughulikiwa awali kama mishipa,tezi na nyenginezo kutokana na changamoto ya fedha, ziliweza kufanikishwa kikamilifu na kutoa afueni kubwa kwa wagonjwa huku huduma hizi zikifaidi idadi kubwa ya wakazi wa Kilifi.
Shukrani za dhati kwa wote waliohusika kufanikisha matibabu haya, wakiongozwa na Kenya Airports Authority(KAA), Fly Jambojet na Mater Misericordie Hospital na tutaendelea kushirkiana na ma shirika mbalimbali ili tuzidi kuboresha huduma za afya kwa faida ya mkazi wa eneo hili.