Wakazi wa Kirumbi, Mnyenzeni, Tsangatsini na maeneo yote yaliyo karibu nao huko Kaloleni, sasa tumewaunganisha na huduma za maji ambazo wamekuwa wakizikosa kwa muda mrefu.
Ni wajibu wangu kama Gavana kuhakikisha wakazi wa Kilifi wanapata huduma bora za maji yaliyo safi na salama na chini ya uongozi wangu, naamini kila kona ya kaunti hii, tutawasambazia maji hadi kwa milango yenu, maana ni haki yenu.