Nafurahi kutangaza ushirikiano baina ya kaunti na kampuni ya Kitui Maize Millers Limited ambayo inataka kufanya mashindano ya soka ya Kilifi Dola Super Cup kwa vijana wetu wapenda kandanda. Mashindano haya yanalenga kukuza talanta na maskauti mbalimbali wakiwemo wa klabu ya soka ya Bandari FC watafuatilia kwa karibu kutambua vipaji vya kipekee.
Ufunguzi rasmi utafanyika tarehe 27 mwezi huu ambapo timu nane za wavulana pekee zilizochaguliwa kutoka kila eneo bunge zitashiriki na mshindi ataiwakilisha Kilifi kwenye fainali za eneo la Pwani zitakazoandaliwa Mombasa, mshindi akitia kibindoni Shillingi millioni moja.
Wakati huu tukiwa kwa mara ya kwanza tunaenda kuanza ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo, kama kaunti, tutaendelea kushirikiana na mashirika, kampuni na wafadhili ili kuhakikisha talanta za michezo zinatambulika na kupata mazingira mazuri ya ukuaji wake.
Tayari tumekuwa na mashindano ya governor’s cup ambayo yamechangia pakubwa kwa ukuzaji wa talanta Kaunti ya Kilifi.
Shukran za dhati kwa Dola kupitia kwa Msimamizi mkuu wa kitengo cha mauzo, Saddam Suleiman na Naibu mwenyekiti wa klabu ya Bandari Twaha Mbarak kwa fursa hii.