KIBAO CHA FUNDISA – ADU ROAD
Tulipokuwa nyanjani kuwaskiza, baadhi ya sauti zenu zilisema, tuendelee kuweka lami barabara ya Kibao Cha fundisa kwenda hadi Adu Kamale huko Magarini. Huu ndio urembo unaoendelea kwa sasa katika barabara hiyo.
Barabara hii itasaidia wakulima wetu wanaosafirisha mazao yao kutoka shambani na kuboresha usafiri wa wakazi wa Magarini kwa jumla. Ni Mung’aro wa Kilifi ambao unaingia hadi vijijini, na kazi bado kwani mkoko ndio unaalika maua maana Mung’aro huu lazima upapaswe kila pembe ya Kilifi.