Kazi kazini . Madunguni ni moja kati ya maeneo yanayozalisha chakula kwa wingi hapa Kilifi. Tulikubaliana nao kwamba tutaweka lami barabara ya Kibao Cha Goshi hadi Madunguni ili kurahisisha usafiri wa mazao yao ya shambani. Kwa sasa kazi inaendelea, kazi ya kung’arisha barabara hiyo.
Tunapomaliza ujenzi wa barabara hii, tayari tumeanza kuchimba visima vya unyunyiziaji maji mashamba eneo hilo, lengo ni kuhakikisha wakulima wanazalisha chakula katika kila msimu na usafirishaji wake uwe umeimarika.