Nimetembelea eneo la Madumadu, Wadi ya Jilore katika barabara ya Sala Gate, nikitathmini uharibifu wa mali na mashamba uliosababishwa na mafuriko.
Nimeweza kukutana na baadhi ya wakazi walioathirika, kuwatahadharisha dhidi ya hatari ya mafuriko na pia nikaweza kuwapa chakula ambacho kitawakidhi kwa muda huu ambao hakuna mazao yoyote shambani. Maafisa wangu vile vile watatoa msaada wa neti na hata malazi ya muda kwa wale ambao makazi yao yamesombwa na maji.