Elimu ya dini ni msingi muhimu katika malezi na makuzi ya watoto wetu, ikilenga kumjua Mungu, kuimarisha maadili, na kukuza utu mwema.
Nimehudhiria mashindano ya kuhifadhi Kitabu Tukufu cha Allah, Quran, yaliyoleta pamoja washindani 160, yaliyofanyika ukumbi wa Nidhamia, Malindi, chini ya udhamini wa Baraza la Muungano na Ustawi wa Walimu wa Madrasa na Wahubiri wa Kiislamu, Kaunti ndogo ya Malindi. Ahmed AbdulRashid kutoka Markaz Muumin ametangazwa mshindi kwa uwezo wake wa kuhifadhi msahafu wote.
Vipaji hivi vinafaa kuendelezwa kwa ajili ya maendeleo bora ya vijana, jamii, na taifa kwa ujumla. Tunatoa pongezi kwa washindi na wote walioshiriki kufanikisha hafla hii.
Nimeandamana na Gavana Abdulswamad Shariff Nassir ( Mombasa), Idris Dokota ( Katibu Baraza la Mawazri), Hon. Amina Mnyazi – M.P Malindi Hon.Paul Katana ( M.P Kaloleni),Sheikh Juma Ngao(Mwenyekiti KEMNAC) miongoni mwa viongozi wengine .