Nimefanya mazungumzo na maafisa wa halmashauri ya ndege Nchini (KAA), wakiongozwa na Robinson Malemo, kujadiliana kuhusu kambi ya siku mbili ya matibabu ya bure itakayofanyika katika chuo cha Kenya Medical Training College (KMTC), Ijumaa na Jumamosi mjini Kilifi.
Kando na KAA, aidha, tumeshirikiana pamoja na Hospitali ya Mater ili kutoa huduma hizi ambazo zitajumuisha upasuaji, tiba ya magonjwa ya macho, kufanyiwa vipimo vya magonjwa ya kisukari, saratani na shinikizo la damu mwilini huku pia madaktari wakichukua data ya watoto walio na matatizo ya ugonjwa wa moyo na baadaye kupewa matibabu ya bure.