“Ashukuriwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja zote. Yeye anatufariji katika mateso yetu yote ili tuweze kuwafariji wale walio katika mateso yao yote, tukitumia faraja ambayo sisi tumepokea kutoka kwa Mungu.”
Rambirambi zangu za dhati kwa familia ya Mzee Shadrack Thoya, Bandarini, Chumani kufuatia kifo cha mpendwa wetu marehemu Bi. Grace Dama Thoya. Marehemu atakumbukwa kwa ushauri wake wa hekma, mpenda maendeleo, kiongozi shupavu na zaidi ya yote mcha Mungu na mshirika mwaminifu wa kanisa la Emmanuel Frere town – Kengeleni.
Kwa dada yangu Evelyn Mwamure, pata faraja katika upendo na kumbukumbu ulizoshiriki na Wifi yako mpendwa. Sina maneno yanayoweza kupunguza kikamilifu maumivu unayopitia na familia yako na kwa niaba ya familia yangu na Gavana Gideon Maitha Mung’aro, pokeeni rambirambi zetu za dhati na mjue kuwa mko kwenye mawazo na maombi yetu katika wakati huu mgumu wa msiba.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Grace Dama Thoya mahali pema peponi. Amina.