Mapema leo nilihudhuria hafla ya mazishi ya marehemu Mama Linnah Mkasi Buni katika eneo la Majengo Kanamai, Wadi ya Mtepeni-Kilifi Kusini.
Marehemu Linnah Buni atakumbukwa kama Mama mcha Mungu, mpenda maendeleo, kiongozi mkakamavu aliyewahi kuwa Diwani mteule na vile vile kuhudumu kama mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Shirikisho.
Kwa familia ya Mzee Buni, jamaa na marafiki wa marehemu, pokeeni salamu zangu za rambirambi, na za Gavana Gideon Maitha Mung’aro kwa kuondokewa na mpendwa wenu. Mwenyezi Mungu awape subra wakati huu wa msiba na mzidi kuweka tumaini lenu kwake akiwa ndiye mfariji wa karibu wakati wa majonzi.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Linnah Mkasi Buni mahali pema peponi. Amina.