Kama tunaishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana; na pia kama tukifa tunakufa kwa ajili ya Bwana. Kwa hiyo basi, kama tunaishi au kama tunakufa, sisi ni mali ya Bwana. – Warumi 14:8
Niliungana na waombolezaji wakiwemo familia, jamaa na marafiki wa mwenda zake Mama Suzan Kudodola Bebora nyumbani kwao Magombe kwa Bebora, Mazeras, eneo bunge la Rabai.
Mwenda zake atakumbukwa kwa kuwa mcha Mungu, kielelezo chema, mwenye upendo na vile vile mama mkakamavu aliyethamini amani na ustawi wa jamii aliyoishi. Kwa niaba ya Gavana Gideon Maitha Mung’aro na familia yangu, tunatoa rambirambi kwa familia kwa kuondokewa na mpendwa wenu.
Tunawaombea faraja na amani itokayo kwa Mwenyezi Mungu na mzidi kumtumaini yeye kwa kila jambo wakati huu wa msiba na mnapofanya matayarisho ya hafla ya mazishi hapo kesho.
Pumzika katika amani ya Mungu Mama Suzan Kudodola Bebora.