Magavana wote wa Pwani, Maseneta, Wabunge wa kitaifa, Wawakilishi Wadi wa kaunti zote sita za eneo hili, viongozi wa kidini, mashirika ya kijamii, kwa sasa tumejumuika pamoja kwenye kongamano kutoa kauli yetu ya mwisho kuhusu marufuku tuliyoweka ya utumizi wa muguka na mihadarati hapa Pwani. Msimamo utakaotolewa hapa, utakuwa ni msimamo wetu kama Wapwani.