Pwani tumesema hatuutaki muguka. Huo ndio msimamo wetu iwe asubui, mchana, jioni au hata usiku. Naamini tukiendelea kushikana pamoja hivi kama viongozi wa eneo hili, Pwani itaheshimika na tutapiga hatua si kwa maendeleo tu, bali pia kwa maswala yanayowaathiri wakazi wa Pwani.