Imenipa furaha kubwa kutangamana na wanafunzi, wakazi na viongozi mbali mbali kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa katika shule ya upili ya wasichana ya Kombeni, Rabai, ambayo jengo la sasa wanalokaa walimu ndilo nililozaliwa, miaka hiyo likitumika kama zahanati.
Kama zawadi yangu wakati naposherehekea siku hii, nitahakikisha tumejenga ua ili kuipa ulinzi shule hii, na tayari nimetuma mhandisi na Afisa Mkuu wa idara ya maji, kuchimba visima vitakavyosambaza maji kwa saa 24 ndani ya shule hiyo. Aidha, kwa zahanati ya sasa ya Kombeni, tunaenda kuibadilisha na kuwa ya kisasa kwa kubadilisha miundombinu yake na hata utoaji wa huduma zake.