Tunapoungana na ulimwengu kusherehekea siku ya Ushirika, ninafurahia kwamba usajili wa vyama vya ushirika unaongezeka kwa kasi mno katika kaunti ya Kilifi. Jumla ya vyama 383 tayari vimesajiliwa, 43 kati ya hivyo vikiwa vimeandikishwa katika mwaka wa kifedha uliokamilika hivi majuzi wa 2023-2024.
Kama serikali ya kaunti, tunaharakisha mchakato wa kuidhinisha mswada wa ushirika wa Kaunti ya Kilifi. Mswada huu utasaidia katika kuimarisha utawala bora utakaoweka mazingira mazuri kwa vyama vya Ushirika kustawi zaidi. Kwa bodaboda, nawasisitiza mjiunge kwa wingi katika Saccos ili malipo ya leseni ya shillingi 300 kila mwezi ambayo sasa hatumlipishi, mujiwekee akiba.