Governors Commitment and Plan
Twende Kilifi
Kilifi NGO Portal
Kazi Kilifi
Buy and Rent – Kilifi

Copyright 2024
Kilifi County Government
Karibu Kilifi

Back
Executive > Tutengeneza taa barabarani

Tutengeneza taa barabarani

Company
Nimezindua gari la Kaunti la kutengeneza taa za barabarani. Gari hili la gharama ya Shilingi milioni 16, litatumika kurekebisha taa za barabarani hasa katika miji yetu mikuu na hata katika taa za milingoti zilizoko vijijini.
Sasa hatuna haja ya kusubiri wanakandarasi kushughulikia taa zetu. Kupitia gari hili, tunaamini swala la giza kutanda nyakati za usiku kutokana na kuharibika kwa taa, tumelizika katika kaburi la sahau na hilo litachangia pakubwa kuimarisha biashara zetu kwa saa 24.
Ni jukumu la serikali ya kaunti ya Kilifi kuhakikisha uwekaji na utengezaji wa taa za umma barabarani na vituo mbalimbali vya biashara ambavyo vimeongezeka kwa kiwango kikubwa. Katika bajeti, tayari tumetenga Shilingi milioni 50 kuendeleza juhudi hizi.
Kilifi itang’ara!
Avatar
Editor@kilifi.go.ke
Date

June 28, 2024

error: Content is protected !!