Tuko na ramani ya barabara zote zinazostahili kuwekwa cabro katika maeneo bunge yote saba ya Kilifi, na kazi kwa sasa inaendelea. Tumemaliza kuweka cabro baadhi ya barabara huko Mariakani, Maisha Bora na Mwakamsha huko Junju, Lake Oil Texas huko Shimo La Tewa, Kurawa- Kwa Chocha mjini Malindi, na nyengine nyingi zinaendelea kukamilishwa.
Barabara hizi sasa tutaziweka taa na kukarabati zile zilizoharibika, maana ni jukumu langu kuhakikisha Kilifi ina metameta iwe usiku au mchana, na mwenye macho ataona Kilifi iking’ara. Lengo ni kuimarisha usafiri na usalama wa ndani wa miji yetu ya Kilifi.