Nimekutana na viongozi wa muungano wa bodaboda kaunti ya Kilifi, wakiongozwa na mwenyekiti wao Khamisi Katambo na kujadiliana maswala muhimu ya jinsi tutapiga jeki sekta hiyo ambayo imeajiri zaidi ya vijana 10,000 Kilifi.
Kati ya tuliyokubaliana ni pamoja na kuwatengezea ofisi, kuwalipia mafunzo ya udereva yatakayowawezesha kupata vibali hitajika baada ya kuhitimu, kuwanunulia vifaa vitakavyowakinga dhidi ya ajali na kama nilivyowaahidi, nitaajiri baadhi yao kuhudumu katika serikali ya kaunti.
Aidha, natoa onyo kali kwa maafisa wa mjini Malindi wanaoendelea kuwatoza bodaboda ada ya maegesho ya kila mwezi baada ya kugundua kwamba, agizo nililotoa hapo awali ya bodaboda wote kutolipishwa ada hiyo limekiukwa huko Malindi pekee. Tulikubaliana pesa yao ya kila mwezi wataweka kwa Saccos ili iwasaidie wao wenyewe, na hilo lazima litekelezwe kikamilifu.