Ahsanteni sana wakazi Kaloleni kwa kujitokeza kwa wingi na kutoa mapendekezo yenu, hakika tutayafanyia kazi kama serikali ya kaunti; kuanzia ujenzi wa Hospitali ya St Lukes ambao tumeauanza, kufungua masoko, kuwaunganisha na maji safi pamoja na kupanua barabara zaidi, hayo wala msitie shaka, tutayatekeleza.
Shukran za dhati kwa Wawakilishi Wadi wote ambao mumeendelea kushirikiana nasi katika safari hii, na kwa Mbunge wa Kaloleni, Mheshimiwa Paul Katana, asante kwa kufika na kushiriki nasi ,vile vile kuyaskia matakwa ya wana Kaloleni, naamini nguvu zako na za Wabunge wengine wa kaunti yetu, tukiendelea kuziweka pamoja, zitamfaidi mkazi wa Kilifi, maana hilo ndilo jukumu letu kama viongozi.