Nimefanya mazungumzo na baadhi ya wakazi wa Wadi ya Mwanamwinga, Kaloleni, wakiongozwa na Mwakilishi Wadi wao, Mheshimiwa Edward Ziro, kuhusu kuboreshwa kwa miundo mbinu eneo hilo.
Uharibifu wa barabara kutokana na mvua inayonyesha, ukosefu wa maji na kuzinduliwa kwa kituo cha afya cha Kithengwani, yalikuwa baadhi ya maswala wanayopendekeza kushughulikiwa kwa jamii hiyo.
Tayari idara husika zinatekeleza baadhi ya hoja zao na naamini kwa ushirikiano huu na wananchi, tunaendelea kutoa suluhu kwa baadhi ya changamoto zinazowakumba wakazi wa Kilifi.