Kufuatia wito wa jamii ya eneo la Rabai, mapema leo, nimekutana na kushauriana na baadhi ya viongozi wa nyanjani eneo hilo, kuhusu maswala muhimu yanayowaathiri kama vile kutatua swala la uhaba wa maji na kuboresha miundomsingi ya Hospitali na shule za chekechea.
Chini ya Simon Makame aliyeongoza kamati ya viongozi hao, nimewahakikishia ushirikiano wangu katika kuhakikisha tunatatua changamoto zinazowakumba wakazi wa Rabai, hasa katika swala la kuboresha idara ya afya, barabara na hata kutoa nafasi za ajira zaidi kwa vijana.
Aidha, viongozi hao wameahidi kushirikiana nami ili kuhakikisha chama cha ODM kinapata uungwaji mkono mkubwa zaidi katika eneo bunge la Rabai, na kama Gavana, nimewasihi kudumisha umoja wakati napotembea nao bega kwa bega katika kufanikisha shughuli zote za kujenga nyumba ya ODM.