Governors Commitment and Plan
Twende Kilifi
Kilifi NGO Portal
Kazi Kilifi
Buy and Rent – Kilifi

Copyright 2024
Kilifi County Government
Karibu Kilifi

Back
Executive > Kilifi Kusini

Kilifi Kusini

Company
Wakazi wa eneo bunge la Kilifi Kusini, tumefurahia kukutana nanyi na kusikiliza vilio vyenu. Bila shaka, ni wazi kwamba baadhi ya mabwenyenye bado wanaendelea kuwahangaisha kuhusu suala la ardhi. Narudia tena, kazi ya maafisa wa polisi si kuwahangaisha wananchi. Kama kuna tatizo lolote, idara husika ziwasiliane na afisi yangu kwanza. Kwa maafisa wachache wanaotumika vibaya, mkome, maana sitaendelea kukubali unyanyasaji unaofanyiwa wakazi wa Kilifi.
Kupitia gazeti rasmi la serikali, tutatangaza kamati ya ardhi ambayo itachaguliwa na kuanza kazi rasmi juma lijalo. Kamati hii, ikishirikiana na afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Kaunti, itapitia shamba hadi shamba na kunakili ripoti kamili kuhusu utata uliopo. Kwa wale mlionyakua ardhi za umma, tunawaonya kwamba kivyovyote vile, mashamba hayo tutayarejesha kwa wananchi na hivi karibuni tutaanza kuvunja baadhi ya nyumba zilizojengwa kwenye ardhi ya umma.
Masuala ya sekta za afya, elimu, barabara, biashara, kilimo, na mengineyo, tumeyanakili na tutayafanyia kazi kikamilifu. Tuendelee kushirikiana ili tuipeleke Kilifi mbele.
Avatar
Editor@kilifi.go.ke
Date

April 20, 2024

error: Content is protected !!